Mafuriko yamesomba makaburi

Mafuriko yamesomba makaburi katikati mwa jiji la GALKAYO nchini SOMALIA na kuacha miili ikielea mitaani
Kulingana na Shirika la Utangazaji la UINGEREZA – BBC, mafuriko hayo ni mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini SOMALIA katika karne moja.

Kuonekana kwa miili iliyofukuliwa na mafuriko kumewatisha wakazi wanaoishi karibu na makaburi huku nyumba zikiwa zimezama kwa kiasi na mabaki ya binadamu yakielea na kuzua hofu ya mlipuko wa magonjwa.

Baadhi ya miili hiyo ilitambulika na kusababisha hofu zaidi na maji yanapopungua mifupa iliyofukuliwa pia huonekana.

Karibu watu 32 wamekufa nchini humo huku Umoja wa Mataifa ukionya kuwa zaidi ya watu milioni moja wanaweza kuathiriwa na mafuriko makubwa ambayo yanakuja baada ya SOMALIA kukumbwa na ukame wa miaka mingi.

Leave a Reply

Your email address will not be published.