MAAMBUKIZI YA MALARIA KWA WATOTO

Kiwango cha maambukizi ya Malaria kwa mkoa wa Tabora kwa watoto wenye umri wa miezi 6 hadi 59 kimeongezeka kutoka 11.7% 2017/2018 hadi kufikia 23.4% mwaka 2022.

Akisoma taarifa hiyo kwa kamati ya bunge ya Afua na UKIMWI mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda  Burian amesema ongezeko hilo ni karibu na mara tatu ya kiwango cha maambukizi kitaifa ambayo ni 8.1% na hivyo kuufanya mkoa wa Tabora kuongoza kitaifa kwa kuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi ya malaria.

Dkt.Batilda Amesema Baadhi ya Changamoto zinazosababisha Mkoa wa Tabora kuendelea kuwa na kiwango cha juu Cha maambukizi ya Malaria ni uwepo wa shughuli za Kilimo zinapelekea ongezeko la mazalia ya mbu akitolea mfano kilimo cha Mpunga kuwa na majaruba mengi yenye maji na Bustani katika maeneo mbalimbali.

Aidha amesema Imani potofu iliyojengeka kwenye jamii juu ya matumizi ya vyandarua vyenye dawa, inachingia  baadhi ya wananchi kutotumia vyandarua wanavyogawiwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya na hivyo Mkoa kuwa na kiwango cha chini cha matumizi ya vyandarua katika Kaya kwa 78% utafiti wa mwaka 2022.

Vilevile Dkt. Batilda amesema mkoa wa Tabora haujawahi kuingizwa kwenye mpango wa Taifa wa kupulizia dawa za ukoko katika nyumba za watu ambayo ni afua yenye kiwango cha juu cha kutokomeza mbu katika makazi ya watu kwa maeneo ya vijijini.

Leave a Reply

Your email address will not be published.