MAJESHI YAUNGANA KUTOA ELIMU KWA JAMII-TABORA

Jeshi la polisi mkoa wa Tabora limeungana na majeshi mengine na kutoa elimu katika shule za Msingi  saba  (7) za Manispaa ya Tabora  kwa kushirikiana na Jeshi la wananchi-JWTZ, Zimamoto  Uhamiaji  pamoja na Jeshi la Magereza.

Mrakibu Mwandamizi wa Polisi  (SSP) Evodius Kasigwa ametoa elimu kwa Wanafunzi hao juu ya  ukatili na unyanyasaji kwa watoto pamoja na namna ya kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi juu ya vitendo vya kikatili watakavyofanyiwa.

Aidha  wanafunzi hao wameweza kupewa elimu kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania   juu ya matukio ya  ugaidi na kuweza kujua ugaidi ni nini, viashiria vya ugaidi kuanzia majumbani, mitaani mpaka mashuleni na ni wapi watoe taarifa endapo wataona viashiria ama dalilili za ugaidi.

Maafisa  kutoka Jeshi la uhamiaji wametoa elimu juu ya wahamiaji haramu ambao wanaingia nchini kwa malengo mabaya.

Jeshi la Magereza wao  walitoa elimu juu ya swala zima la kurekebisha nidhamu kwa wale wanaokiuka maadili na taratibu za kisheria.

Kwa Upande wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji  walitoa elimu juu ya kupambana na majanga ya moto na ni vitu gani kama watoto hawapaswi kuvitumia ambavyo vinaweza kusababisha moto majumbani.

Leave a Reply

Your email address will not be published.