Wanigeria 170 wamerudishwa nyumbani 

Zaidi ya Wanigeria 170 waliokuwa kwenye ndege kuelekea SAUDI ARABIA wamerudishwa nyumbani baada ya mamlaka ya SAUDIA kuripotiwa kufutilia mbali viza zao
Vyombo vya habari vya NIGERIA vimeripoti kuwa abiria 264 ambao walikuwa wameondoka katika miji ya LAGOS na KANO walipokea viza na kufanyiwa uchunguzi mkali kabla ya kupanda ndege.
Hata hivyo,viza zao zote ziliripotiwa kufutwa wakiwa angani.
Walipofika, mamlaka ya SAUDIA iliripotiwa kukataa kuwaruhusu kuingia na kuamuru shirika la ndege la Air Peace la NIGERIA kuwarejesha nyumbani NIGERIA.
Mamlaka ya Saudia haijazungumzia suala hilo.
Abiria walioathiriwa wameviambia vyombo vya habari vya ndani kwamba walishangaa kusikia kuhusu kukataliwa kwa viza walipotua kwa sababu walikuwa wamekidhi mahitaji yote ya kuingia katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.
SAUDI ARABIA inasemekana hatimaye iliruhusu kuingia kwa abiria 87 baada ya Balozi wa NIGERIA nchini humo kuingilia kati,lakini 177 wamerejeshwa

Leave a Reply

Your email address will not be published.