MADIWANI URAMBO WASHUSHA

Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Urambo mkoani Tabora limeazimia kuwafukuza kazi watumishi wa afya wawili na wengine wawili kushushiwa mishahara baada ya kukutwa na hatia ya makosa mbalimbali.

Mwenyekiti wa wa halmashauri hiyo Adam Malunkwi amesema baada ya baraza kukaa kama kamati na limewaazimia watumishi hao Palestina Emmanuel muuguzi daraja la pili na Ally Saidi afisa muuguzi msaidizi daraja la kwanza kwa makosa ya utoro kazini.

Pia baraza limeazimia kushushiwa mshahara watumishi wawili David Salumu ambaye ni muuguzi mkuu msadizi kwa kulewa kazini na kumpunguzia asilimia 15 ya mshahara wake kwa  miaka mitatu bila kupanda cheo.

Amesema mwingine ni Patrick Ghati ambaye ni afisa afya mazingira msaidizi daraja la pili kwa kosa la kuzibua mirija ya uzazi kunyume na taaluma yake.

Mwezi August mwaka huu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Urambo Grace Quntine aliunda tume ya uchunguzi baada ya kuongezeka malalamiko kutoka kwa wagonjwa yakiwalenga watoa huduma wa afya.

Leave a Reply

Your email address will not be published.