HAMAS na ISRAEL

PALESTINA tunaarifiwa kuwa watoto 24 waliozaliwa kabla ya muda nchini PALESTINA kutokana na vita vya kundi la HAMAS na ISRAEL wamehamishwa kutoka hospitali ya AL SHIFA na kupelekwa eneo ambalo umeme unapatikana ili kuona namna ya kupigania uhai wao
Kwa mujibu wa Mwandishi wa habari wa runinga ya ALJAZEERA,HANI MAHMOUD zoezi hilo bado linakumbwa na changamoto kutokana na watoto hao kutokuwa kwenye vifaa vya kutunzia watoto waliozaliwa kabla ya muda kwa sababu mapigano yanayoendelea yameharibu miuondombinu ya hospitali.
Muuguzi mmoja katika hospitali ya AL-AQSA MARTYRS katika mji wa Gaza amesema kumekuwa na ongezeko la watoto wanaohitaji uangalizi wa karibu,lakini uangalizi huo unashindikana kutokana na ISRAEL kuendelea kuyashambulia maeneo ya umma.
Hospitali za mji wa GAZA zimeshindwa kuendesha shughuli zake kama inavyotakiwa hivi karibuni kutokana na ISRAEL kuzidisha mashambulizi kwenye maeneo ya umma inayoamini kuwa yanakaliwa na maadui zao kundi la HAMAS.

Leave a Reply

Your email address will not be published.