Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora

Mkuu wa mkoa wa Tabora amemuagiza kufika ofini kwake mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya Masasi Constraction anayesimamia ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya rufaa ya mkoa Kitete baada ya kutoridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo.

Akizungumza baada ya ukaguzi wa jengo hilo, Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Burian amesema hajaridhishwa na viwango vya ubora na kasi ya kazi katika jengo hilo ambalo lilipaswa kukamilika mwezi September mwaka huu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora -Kitete Mark Waziri amesema changamoto iliyokuwa inaukabili mradi huo wa ujenzi ni ucheleweshwaji wa fedha kwa mkandarasi.

Ujenzi wa jengo la mama na mtoto ulioanza mwaka 2022, unatarajiwa kukamilika December mwaka huu na pindi ukikamilika, jengo litawahudumia wazazi 400 kwa wakati mmoja.

Nini maoni yako?

Leave a Reply

Your email address will not be published.